ACT kufanya kikao cha halmashauri kuu Jumapili

Habari Leo
Published: Feb 21, 2025 14:14:08 EAT   |  General

DAR ES SALAAM: CHAMA cha ACT – Wazalendo kimeeleza kuwa kitafanya kikao chake cha Halmashauri Kuu Februari 23,…

The post ACT kufanya kikao cha halmashauri kuu Jumapili appeared first on HabariLeo.

DAR ES SALAAM: CHAMA cha ACT – Wazalendo kimeeleza kuwa kitafanya kikao chake cha Halmashauri Kuu Februari 23, 2025 ukumbi wa Hakainde Hichilema uliopo jengo la Maalim Seif, Magomeni Dar es salaam.

Taarifa iliyotolewa leo Februari 21, 2025 na Naibu Katibu Idara ya Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma, Shangwe Ayo imefafanua kuwa pamoja na mambo mengine, Halmashauri Kuu inatarajia kupokea taarifa ya kina ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024.

SOMA ZAIDI: ACT kujadili uchaguzi mitaa

Taarifa ya Shangwe imesema wajumbe watafanya tathmini kwa kina kuhusu uchaguzi huo na kutoa maagizo kwa chama juu ya hatua muafaka za kuchukua.

Halmashauri Kuu pia, itajadili na kutoa mwelekeo wa chama kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

“Halmashauri Kuu ni kikao cha pili kwa ukubwa na kimadaraka cha ACT Wazalendo, baada ya Mkutano Mkuu. Mbali na wajumbe wa kuchaguliwa, Halmashauri Kuu inaundwa na wenyeviti na makatibu wa mikoa yote ya kichama nchini, Bara na Zanzibar. Kikao cha Halmashauri Kuu kitatanguliwa na Kamati Kuu ambayo itakutana tarehe 22 Februari, 2025 Makao Makuu ya Chama,” imeeleza taarifa hiyo.

The post ACT kufanya kikao cha halmashauri kuu Jumapili appeared first on HabariLeo.