Abdulla: Filamu ya Royal Tour imeongeza watalii 183%
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla amesema filamu ya The Tanzania…
The post Abdulla: Filamu ya Royal Tour imeongeza watalii 183% appeared first on HabariLeo.
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla amesema filamu ya The Tanzania Royal Tour imechangia sekta ya utalii kuchangia pato la taifa kwa asilimia 30 huku watalii wakiongezeka kwa asilimia 183.
Abdulla aliyasema hayo jana wakati wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuanzia Novemba, 2020 hadi Desemba, 2024 kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM Taifa.
Alisema mchango wa utalii katika Pato la Taifa umefikia asilimia 30 huku idadi ya watalii imeongezeka kutoka 260,644 mwaka 2020 hadi kufikia 736,755 mwaka 2024 sawa na ongezeko la asilimia 183.
Alisema mafanikio hayo yamechangiwa kutokana na kazi ya uandaaji wa filamu na makala ya kuutangaza utalii ya The Tanzania Royal Tour ambayo iliongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan na kuvitangaza vivutio vya utalii vya Tanzania Bara na Zanzibar.
Pia, kuboreshwa kwa miundombinu, mawasiliano na uwekezaji wa hoteli za kisasa ambapo miradi ya maendeleo ya utalii imeongezeka kutoka 995 mpaka 1,695.
Aidha, serikali inaendelea kukifungua Kisiwa cha Pemba kwa utalii kwa kuvutia wawekezaji katika sekta hiyo. Abdulla alisema katika masuala ya mambo ya kale na utunzaji kumbukumbu za taifa na uhifadhi na uen[1]delezaji wa urithi wa dunia, serikali imetekeleza mradi wa kuweka miundombinu ya maji, umeme na mawasiliano chini ya ardhi.
Pia, kusimamia ujenzi wa awamu ya pili ya mradi wa Darajani Souk ambao unahusisha maduka na ofisi, ujenzi wa maegesho ya Malindi, kufanya ukarabarati wa Soko kuu la Darajani, kufanya matengenezo katika maeneo ya kihistoria ya Mnazi Mmoja na matengenezo ya Kaburi la Tip Tipp lililopo Shangani.
The post Abdulla: Filamu ya Royal Tour imeongeza watalii 183% appeared first on HabariLeo.