ZARAA: Atambua vinyonga ni dawa ya wadudu shambani

NA SAMMY WAWERU SHAMBA la Charles Mburu ni bustani ya mseto wa matunda, mengi akiwa anayakuza kwa minajili ya biashara. Limesheheni matunda kama avokado, ndizi, machungwa, mapapai, mapera, matundadamu, matikiti ya pepino, karakara, stroberi, matufaha, zabibu, maembe, komamanga na ndimu.Mburu anasema ana zaidi ya aina 20 ya matunda, katika shamba lake lililoko Ndeiya, Kaunti ya […]