Waziri Kindiki: Shakahola ina makaburi mengi

NA SAMMY WAWERU ENEO la Shakahola, Kilifi lingali na makaburi mengi, ametangaza Waziri wa Usalama wa Ndani Prof Kithure Kindiki. Kwenye hotuba yake kwa taifa Jumatano, Mei 31, 2023, Waziri amesema shughuli ya ufukuaji maiti zaidi zilizozikwa itaanza Jumatatu ijayo, Juni 5, 2023. “Makaburi yangali mengi Shakahola na ufukuaji miili utaanza Jumatatu, wiki ijayo,” akasema […]