Uhuru ataacha deni la ahadi alizotoa kwenye kampeni- Ruto

Na WYCLIFFE NYABERI NAIBU Rais Dkt William Ruto amemshambulia Rais Uhuru Kenyatta huku akisema ataondoka mamlakani bila kulipa deni la ahadi alizotoa kwa Wakenya. Dkt Ruto alitumia ziara yake Kisii, kukosoa Rais Kenyatta kuhusu ajenda nne kuu za maendeleo ambazo alisema utekelezaji wake utasalia kuwa ndoto.