Uhuru arejesha Jamhuri eneo ilikoanzia

Na WANDERI KAMAU RAIS Uhuru Kenyatta jana Jumapili alirejesha maadhimisho ya sherehe za Sikukuu ya Jamhuri katika Bustani ya Uhuru, Nairobi, ambako zilifanyika kwa mara ya kwanza Kenya ikianza kujitawala Desemba 12 1964. Kwenye hotuba yake, Rais Kenyatta alisema hatua hiyo inalenga kuwafahamisha Wakenya kuhusu safari ambayo Kenya imepiga ili kufikia iliko. “Hili linalenga kutukumbusha […]