TAHARIRI: Naibu Rais awafichue wafisadi wote

NA MHARIRI UFISADI umekuwa maradhi yanayosababisha uchumi na ustawi wa taifa letu kuendelea kudidimia, kiasi cha viongozi kufeli kushirikiana kupata tiba kamili na ya kudumu. Madhara ya ufisadi ni Wakenya kuteseka kwa kukosa ajira, maendeleo duni, gharama ya juu ya maisha, uchumi uliosambaratika na ukabila katika ajira. Ufisadi pia umechangia miradi mingi muhimu kukwama nchini,kucheleweshwa […]