Raila kujenga hoteli itakayogharimu nusu bilioni Malindi

NA VALENTINE OBARA KAMPUNI inayohusishwa na kiongozi wa ODM Raila Odinga, imepanga kujenga hoteli ya kifahari kwenye ardhi ambayo awali ilikuwa ikizozaniwa Malindi, Kaunti ya Kilifi. Stakabadhi zilizosomwa na Taifa Leo zilionyesha kuwa, kampuni hiyo ya Kango Enterprises Limited ambapo Bw Odinga ni mmoja wa wakurugenzi, itatekeleza ujenzi huo kwenye ardhi ya karibu ekari 4.3. […]