Polisi bandia anayehangaisha wakazi Nairobi

Na RICHARD MUNGUTI MWANAMUME anayejifanya polisi na kuhangaisha wakazi jijini Nairobi amekamatwa na kufunguliwa mashtaka. Polisi bandia huyo aliyetambuliwa kama Stanley Ng’ang’a, alishtakiwa mbele ya hakimu mkazi Mercy Malingu. Ng’ang’a anakabiliwa na shtaka la kukamata mfanyabiashara Nairobi, akijifanya askari. Akisomewa makosa yake mbele ya Hakimu Mercy, alikana kuwatia nguvuni Kenton Ombati pamoja na wafanyakazi wake […]