PAUKWA: Msanii afumaniwa na Kaburu pabaya

NA ENOCK NYARIKI ASUBUHI, Bwana Kaburu aliitembelea Idara ya Parachuti. Kama ilivyokuwa ada, shughuli zilikuwa nyingi huko kuliko kwingineko mbugani. Parachuti zilikwenda juu kwa umahiri mkubwa. Katika kila parachuti aliketi mtalii mmoja na mwelekezi wake ambaye angemwonyesha mtalii mahali salama ambapo wangetua. Watalii wengine walijilaza kwenye viti vya hinzirani idarani hapo huku wakiendelea kuota jua […]