Pasta tapeli wa mashamba taabani

Na RICHARD MUNGUTI PASTA wa Kanisa la Kipendekoste ameshtakiwa kwa kupeli Wakenya watatu wanaoishi Amerika Sh6.8 milioni akidai atawanunulia mashamba jijini Nairobi. Pasta Catherine Wairimu Ng’ang’a wa Arise and Healing and Deliverance Church lililoko eneo la Githurai ameshtakiwa katika Mahakama ya Milimani. Aliposomewa mashtaka manne mbele ya Hakimu Mwandamizi Bi Zainab Abdul Pasta Wairimu alikana kuwalaghai […]