Omtatah awasilisha kesi kupinga Mswada wa Fedha 2023

NA RICHARD MUNGUTI SENETA wa Busia Okiya Omtatah amewasilisha kesi katika Mahakama ya Milimani jijini Nairobi leo Ijumaa akiiomba itie breki Mswada wa Fedha, 2023. Seneta huyo aliyetofautiana hadharani na Rais William Ruto alipozuru Busia, amesema mswada huo unakiuka Katiba.