Kilio mwanamume aliyeenda kusomea Afrika Kusini akiuawa na wateja wake wa teksi

NA KASSIM ADINASI FAMILIA moja ya Muhanda, eneobunge la Gem inataka majibu baada ya kijana wao aliyeenda kusomea nchini Afrika Kusini kuaga dunia katika mazingira tata. Enock Wamare Hosea almaarufu ‘Blacky’ aliyekuwa na umri wa miaka 30, alikuwa akiishi mjini Cape Town nchini Afrika Kusini kwa miaka 11. Alikuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Cape Town […]