Kero ya Ndovu: Wakazi wa Ganze wasumbuka kupata fomu za kujaza walipwe fidia

NA MAUREEN ONGALA MBUNGE wa Ganze Kenneth Kazungu amelitaka Shirika la Huduma kwa Wanyamapori (KWS) kurudisha huduma zake mashinani ili kupunguza mahangaiko ya wananchi ambao makazi yao na mashamba yamevamiwa na ndovu. Amelalamika imekuwa vigumu kwa waathiriwa wa uvamizi wa wanyamapori kupata fidia kwa sababu ya gharama za kusafiri hadi afisi za KWS mjini Malindi. […]