AMINI USIAMINI: Kipepeo anayefahamika kama ‘glasswing butterfly’

NA MWORIA MUCHINA KIPEPEO anayejulikana kama glasswing butterfly au kwa jina la kisayansi Greta oto, huwa na mabawa yenye mwonekano wa glasi (transparent) kumwezesha kufanana na mazingira karibu naye. Hii humwezesha kujificha kutoka kwa maadui wanaoweza kumshambulia na hata kumla. Ni nadra sana kuwatambua vipepeo hao wanapotulia kwenye majani na matawi ya mti.