Msama atekeleza agizo la Waziri Silaa

Habari Leo
Published: Mar 29, 2024 13:24:46 EAT   |  News

DAR ES SALAAM; MKurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama ametekeleza agizo la Waziri wa Ardhi, Jerry Silaa la kwenda kuonana na Kamishina wa Ardhi Kanda ya Dar es Salaam. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Msama amesema alienda jana ofisini kwa Kamishina wa Ardhi na kueleza kuwa kuna maelekezo amepewa …

The post Msama atekeleza agizo la Waziri Silaa first appeared on HabariLeo.

DAR ES SALAAM; MKurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama ametekeleza agizo la Waziri wa Ardhi, Jerry Silaa la kwenda kuonana na Kamishina wa Ardhi Kanda ya Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Msama amesema alienda jana ofisini kwa Kamishina wa Ardhi na kueleza kuwa kuna maelekezo amepewa atayafanya na kwa vile jambo hilo tayari lipo wizarani basi litafanyiwa kazi.

“Waziri wetu ni mtu anayefanya kazi yake vizuri sana na hakika Wizara ya Ardhi imempata mchapa kazi mzuri, nampongeza.

“Lakini nimeona pia nitoe pia ufafanuzi zaidi kuhusu kiwanja kinachozungumziwa kilichopo Kibada wilayani Kigamboni, kiwanja hicho chenye namba DSMT 1022673 sijakivamia ni changu na nakimiliki kihalali.

“Sijawahi kumtapeli mtu kiwanja, nina nyaraka zote za umiliki, nimemilikishwa na Wizara ya Ardhi. Kuhusu kuwa na kiwanja eneo la Mbweni, hicho sikitambui na si changu,” amesema Msama.

Amedai kuwa amesikitishwa na diwani mmoja aliyempa taarifa zisizo sahihi Waziri Silaa kuwa amewatapeli wananchi kiwanja na kusisitiza kuwa maneno hayo hayana ukweli na yanamchafua kwani yeye ni mfanyabiashara wa miaka mingi anayeheshimika.

Amesema wakati mwingine madai ya kuhusishwa na viwanja yanatokana na alipokuwa na Kampuni ya udalali, ambayo ilikuwa ikipewa tenda na mahakama katika masuala ya ardhi.

“Sasa kampuni inaenda kusimamia jambo fulani, kampuni inaitwa Msama watu wanajua mimi ndiye naenda kuchukua ardhi au nyumba,” amesema.

 

The post Msama atekeleza agizo la Waziri Silaa first appeared on HabariLeo.