Kampuni uchimbaji madini yapandikiza vifaranga vya samaki

KAMPUNI ya Diamond Williamson Ltd inayojishughulisha na uchimbaji wa madini ya almas iliyopo Mwadui wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, wamepandikiza vifaranga 5000 vya samaki aina ya Sato katika bwawa jipya la Mwang’olo ili kuinua kipato cha wananchi na chakula. Upandikizaji wa vifaranga vya samaki aina hiyo limefanyika jana tarehe 8,2023 kwa kuzinduliwa na Katibu Tawala wa …
The post Kampuni uchimbaji madini yapandikiza vifaranga vya samaki first appeared on HabariLeo.
KAMPUNI ya Diamond Williamson Ltd inayojishughulisha na uchimbaji wa madini ya almas iliyopo Mwadui wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, wamepandikiza vifaranga 5000 vya samaki aina ya Sato katika bwawa jipya la Mwang’olo ili kuinua kipato cha wananchi na chakula.
Upandikizaji wa vifaranga vya samaki aina hiyo limefanyika jana tarehe 8,2023 kwa kuzinduliwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kishapu Fatma Mohamed akimwakilisha Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude.
Meneja Mahusiano Mgodi wa Almasi, Mwadui Bernard Mihayo akizungumza katika zoezi hilo amesema wametekeleza agizo la serikali la kurudisha kila kitu ambacho kiliharibika baada ya kupasuka kwa bwawa la majitope la mgodi huo Novemba mwaka jana.
Mihayo amesema ulipwaji fidia kwa waathirika limemalizika na sasa wanachofanya ni kurudishia Mazingira ikiwamo upandaji miti na kupandikiza vifaranga vya samaki katika bwawa Jipya ili wananchi waendelee na shughuli zao kama kawaida ikiwamo uvuvi wa samaki
Baada ya kupasuka kwa bwawa la kuhifadhia Majitope, liliathiri Bwawa ambalo wananchi walikuwa akilitumia kufanya shughuli za uvuvi wa Samaki,” amesema Mihayo.
“Baada ya kujenga bwawa hili Jipya katika kijiji cha Mwang’olo,tumetekeleza maagizo ya Serikali na Leo tumekuja kupandikiza vifaranga vya Samaki 5,000 aina ya Sato ili wananchi waendelee na shughuli zao za uvuvi kama zamani,” ameongeza Mihayo.
Aidha, amesema katika zoezi la upandaji miti ili kutunza Mazingira katika vijiji vyote vinayozunguka Mgodi huo kwamba hadi sasa wameshapanda Miti 10,000 na zoezi hilo ni endelevu.
Ofisa Uvuvi wilaya ya Kishapu Moses Ng’winza, ametoa wito kwa wananchi wasubili hadi miezi sita samaki hao watakuwa tayari wamekuwa wakubwa, pamoja na kusubiri maelekezo kutoka Serikalini na kupewa elimu ndipo waanze shughuli za uvuvi.
Katibu Tawala wa wilaya ya Kishapu Fatma Mohamed, ameupongeza mgodi huo wa Mwadui na kuwataka wananchi kulitunza bwawa hilo na kila mmoja awe mlinzi wa mwezake pamoja na kuacha kulima Kando ya bwawa ili samaki hao waje kuwa msaada mkubwa kwao kiuchumi na kupata kitoweo.
Baadhi ya wananchi hao Lucas Moye na Laurent Fabiani wsmesema wanaushukuru Mgodi huo kwa kupandikiza vifaranga vya Samaki katika bwawa jipya, ili warudi katika shughuli zao za uvuvi na kujiongezea kipato.
The post Kampuni uchimbaji madini yapandikiza vifaranga vya samaki first appeared on HabariLeo.