Tanzania, Hungary zasaini mkataba wa ushirikiano sekta ya maji

Mtanzania
Published: Mar 28, 2024 14:45:26 EAT   |  News

Na Esther Mnyika Mtanzania Digital Serikali ya Tanzania na Hungary zimesaini mkataba wa ushirikiano katika sekta ya maji utakaosaidia udhibiti wa mafuriko na maji taka ambao umekuwa changamoto. Ikumbukwe kuwa Hungary inaongoza duniani kwa kudhibiti mafuriko ya maji pamoja na maji taka, hivyo teknolojia hiyo itasaidia kuleta ahueni kwa Tanzania. Mbali na nyanja ya udhibiti […]

Na Esther Mnyika Mtanzania Digital

Serikali ya Tanzania na Hungary zimesaini mkataba wa ushirikiano katika sekta ya maji utakaosaidia udhibiti wa mafuriko na maji taka ambao umekuwa changamoto.

Ikumbukwe kuwa Hungary inaongoza duniani kwa kudhibiti mafuriko ya maji pamoja na maji taka, hivyo teknolojia hiyo itasaidia kuleta ahueni kwa Tanzania.

Mbali na nyanja ya udhibiti wa maji, pia Hungary inatarajia kufanya uwekezaji wa kiwanda cha kutengeneza ndege ndogo mkoani Morogoro.

Akizungumza leo Machi 28, 2024 jijini Dar es Salaam baada ya kusaini mkataba huo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba amesema ugeni huo umekuja baada ya Rais wa Hungary, Katalin Novák, kufanya ziara nchini mwaka jana.

“Tumefanya mazungumzo ya kiserikali ikiwemo ushirikiano wa kibiashara ikihusisha makongamano, hivyo nchi hizi mbili zitakuwa zinafanya ziara za kibiashara kwa sekta binafsi,” amesema Makamba.