Shadrack Monga, Japhet Zabron watoka na ‘Siwezi Amini’

Mtanzania
Published: Apr 19, 2024 10:00:00 EAT   |  Entertainment

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital MWIMBAJI anayekuja kwa kasi kwenye muziki wa Injili kutoka nchini Marekani, Shadrack Monga, amerudi kivingine na wimbo Siwezi Amini akiwa amemshirikisha Japhet Zabron. Monga, amekuwa akijizolea unaarufu kwenye muziki huo kupitia nyimbo zake mbalimbali na sasa hivi amewabariki mashabiki wa Afrika Mashariki kupitia kolabo hiyo. Akizungumza na mtanzania.co.tz Monga amesema […]

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

MWIMBAJI anayekuja kwa kasi kwenye muziki wa Injili kutoka nchini Marekani, Shadrack Monga, amerudi kivingine na wimbo Siwezi Amini akiwa amemshirikisha Japhet Zabron.

Monga, amekuwa akijizolea unaarufu kwenye muziki huo kupitia nyimbo zake mbalimbali na sasa hivi amewabariki mashabiki wa Afrika Mashariki kupitia kolabo hiyo.

Akizungumza na mtanzania.co.tz Monga amesema tayari audio na video ya wimbo huo inapatikana kwenye mitandao mbalimbali hasa chaneli yake ya YouTube.

“Mapokezi ni mazuri, nashukuru video inachezwa kwenye TV kubwa hapo Afrika Mashariki, kiu yangu ni kuona injili inawafikia wengi zaidi,” amesema Monga.