Yanga, Simba zaonywa

Mwanaspoti
Published: Sep 28, 2023 16:32:03 EAT   |  Sports

KAMATI ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi Kuu Bara (TPLB), imetoa onyo kwa timu za Yanga na Simba huku Azam FC na Tabora zikitozwa fedha kwa kutokuzingatia kanuni. Yanga imepewa onyo hilo kwa kosa la kuwakilishwa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi pekee kwenye mkutano na wanahabari kuelekea mchezo na JKT Tanzania vivyo hivyo kwa Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira 'Robertinho' kuwakilishwa nae kwenye mkutano na wanahabari katika mchezo na Coastal Union. "Klabu ya Simba imetozwa faini ya Sh1 milioni kwa kosa la baadhi ya maofisa wake kumfanyia vurugu kiongozi mmoja wa klabu ya Coastal Union katika mchezo tajwa uliofanyika uwanja wa Uhuru," imeeleza taarifa KMC imepewa onyo kufuatia kwa makosa mawili Kocha Mkuu, Abdihamid Moallin na mchezaji Waziri Junior kuchelewa kufika kwenye mkutano na wanahabari na pili kuwakilishwa na maafisa wanne badala ya watano kwenye mkutano wa maandalizi ya mechi yao na Namungo. Tabora United imetozwa kiasi cha Sh1 milionI kwa kosa la mashabiki wake kufanya vurugu na kuzuia basi la Tanzania Prisons nje ya uwanja. Kocha wa magolikipa wa Azam, Khalifa Aboubakar ametozwa kiasi cha Sh 500,000 kwa kosa la kufanya vurugu lango la kuingilia eneo la kuchezea uwanja wa Azam Complex.