Usajili mpya Simba kushtua, Mbrazili ashikilia faili la mastaa wakali

Mwanaspoti
Published: Mar 24, 2023 09:34:15 EAT   |  Sports

SIMBA inaendelea kupiga hesabu za kucheza hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini kocha wa timu hiyo Roberto Oliveira ‘Robertinho’ akili yake iko mbali sana - kuna kazi moja ya kibabe anaifanya itakayowashtua na kuwafurahisha mashabiki wa timu hiyo.