Stars yaichapa Cranes ikiita kwa Mkapa

Stars imebakiza mechi tatu za uamuzi ambapo Jumanne Machi 28 mwaka huu itaikaribisha Uganda katika mechi ya marudiano itakayopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa na baada ya hapo itawakaribisha Niger ambayo katika mechi ya kwanza ililazimishwa sare ya bao 1-1 kwao na Algeria iliyoshinda 2-0 nyumbani.