Simba, Yanga zishikilie 'bomba'

Mwanaspoti
Published: Mar 22, 2023 19:36:24 EAT   |  Sports

OFISA habari wa Simba, Ahmed Ally amesema itakuwa na maana kubwa sana kwa nchini kama klabu za Tanzania ikiwemo Simba na Yanga zitaendelea kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa. Ahmed ambaye alikuwa mmoja wa wachangiaji kwenye Twitter Space ya Mwananchi alisema, "Mpira wa nchi hii umepiga hatua kubwa kwa timu za Simba na Yanga kufuzu robo fainali kwa sababu ni kwa mara ya kwanza lakini pia kuna nchi utaona ina timu moja tu kwenye hii hatua sasa hili ni jukumu letu kubwa la kuhakikisha tunaendelea kushikilia hapa tulipo," "Hii inamaana kuna kazi kubwa imefanyika kuanzia kwenye klabu, wasimamizi na Serikali ingekuwa timu moja pekee, tungesema ni juhudi za Simba pekee mathalani zipo timu mbili basi kuna nguvu kubwa, kwenye 50 akifaulu mmoja ni juhudi za mtu binafsi wakifaulu zaidi lazima useme kuhusu mwalimu," "Robo fainali mbili ni ishara tosha kuwa mpira wetu unapiga hatua huku tukianglia changamoto wapi zilizopo ili kutatua, niwapongeze Yanga kwa uimara, waliamini mafanikio ni kuifunga Simba lakini kwa sasa wameonyesha walilala kwa miaka mingi na sasa wameamka," alisema Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amesema Simba haijawahi kumuamsha Yanga kwenye jambo lolote lile kwa sababu wamefanya mabadiliko makubwa ya kiundeshaji kwenye uongozi hivyo wanajivunia hilo na suala la kuifunga Simba hawataliacha.