Phiri uhakika Simba, wakaa na kocha

Mwanaspoti
Published: Jun 01, 2023 08:31:23 EAT   |  Sports

Zilikuwepo taarifa za straika wa Simba, Moses Phiri kutaka kusepa kutokana na kushindwa kupata nafasi kikosi cha kwanza baada ya kutoka kuuguza majeraha, upepo umebadilika staa huyo ataendelea kusalia Msimbazi. Ipo hivi; Imeelezwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salum Abdallah 'Try Again' alimwita Phiri na kumkalisha chini, ili kumweleza bado wanamhitaji kwenye kikosi, hivyo wakakubaliana kwa amani na sasa staa huyo bado yupo Msimbazi. "Uongozi umemwomba Kocha Roberto Oliviera 'Robertinho' kukaa na staa huyo ili wamalizane vizuri kama ilivyokuwa kwa kiungo Clatous Chama na lengo ni kuona tunaendelea kumuona hapa msimbazi," kilisema chanzo hicho. Alipoulizwa Phiri alisema: "Bado ni mchezaji wa Simba, nina mkataba wa mwaka mmoja baada ya kumalizika msimu huu, msimu ujao bado nitaonekana nikiwa na jezi nyekundu kuitumikia klabu yangu."