Ndemla kuwakosa Mbeya City

KIUNGO wa Singida Big Stars,Said Ndemla anatarajia kuukosa mchezo wa robo fainali ya Kombe la Azam Sports Federation (ASFC) dhidi ya Mbeya City unaotarajiwa kufanyika Aprili 2 mwaka huu katika uwanja wa Liti mkoani Singida.