Nani aondoke?

Mwanaspoti
Published: Jun 01, 2023 08:53:57 EAT   |  Sports

Kwa maoni ya Feisal Salum 'Fei Toto', akihojiwa leo kitup cja luninga cha Clouds TV amesema anaweza kurudi Yanga kama rais wa timu hiyo, Hersi Said ataondoka. Fei Toto amesema; "Rais kama hayupo sasahivi narudi, akiondoka tu sasahivi narudi Yanga," Mei 24 wakati akihojiwa Clouds Tv rais wa Yanga, Hersi Said alisema; “Feisal ni mmoja kati ya Wachezaji bora na wenye nidhamu ambao tumewahi kuwa nao Yanga hadi leo katika wachezaji ambao niliwakuta Yanga, yeye ni mchezaji mkongwe zaidi kati ya wote sababu hakuna yeyote aliyesalia Yanga hadi leo ispokuwa yeye, lakini pia hajawahi kuwa na changamoto yoyote ya kinidhamu, alikuja akiwa mdogo ndio maana akapewa jina la Fei Toto.” “Kama GSM tuliwahi kumwita Feisal na kukaanae kujadili maslahi yake ambayo hayakuwa madogo hata kwa wakati huo, alikuwa akipokea mshahara wa Sh1.5 milioni na tukamuongezea hadi kufikia Sh4 milioni mwezi pamoja ada ya usajili Sh100 milioni, sitaki kwenda mbali ila mimi naamini kuna kitu nyuma ya Feisal kinachomsukuma kufanya haya” Sakata la Fei Toto na Yanga bado limezidi kuchukua sura mpya kwa kutopata muafaka baada ya kushindwa kuvunja mkataba na timu hiyo na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kumtaka kurudi kutumikia mkataba wake unaoisha mwakani.