Mghana wa Singida Big ASatupwa nje

Mwanaspoti
Published: Jun 01, 2023 12:35:35 EAT   |  Sports

KIRAKA wa Singida Big Stars, Nicolas Gyan anaweza kukosa mechi mbili za Ligi Kuu zilizosalia kutokana na kupata majeraha ya nyonga yatakayomweka nje hadi msimu ujao. Gyan amekuwa na kiwango kizuri akicheza kama beki wa kulia katika kikosi hicho huku pia akimudu vyema kucheza kama kiungo mshambuliaji. Mwanaspoti lilipata habari kiraka huyo kwa sasa hafanyi mazoezi na Singida baada ya kupata majeraha na alipotafutwa alikiri ameumia ndio maana hayupo kikosini. "Ndio nimeumia na sina hakika kama nitamaliza hizi mechi mbili kwa sababu ya maumivu niliyonayo, nimeambiwa natakiwa nipate muda mwingi wa kupumzika ili nikae sawa; "Pia baba yangu hayupo sawa (anaumwa) nyumbani (Ghana) kwa hiyo natakiwa niwepo kule." Gyan ambaye aliwahi kuwika na Simba amekuwa na uhakika wa kucheza kikosi cha kwanza mbele ya Paul Godfrey ambaye ndio beki asili kwenye nafasi hiyo kwa sasa.