Mfaume Mfaume apata ajali Singida

Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Mfaume Mfaume 'Mapafu ya Mbwa' amenusurika kifo katika ajali iliyotokea jana mkoani Singida ikihusisha gari yake ilioharibika vibaya. Kwa mujibu wa Msemaji wa kambi ya Team Naccoz, Feiz amesema kuwa ajali hiyo imetokea jana na wote wametoka salama. Ajali hiyo imemuhusisha Mfaume na baadhi ya ndugu zake ambao walikuwa wakielekea Singida katika jambo la kifamilia pamoja na kwenda Mwanza kumsapoti mmoja kati ya mabondia wa Team Naccoz anayetarajia kupigana kesho Ijumaa kwenye pambano la Boxing Royal Tour.