KWA MAYELE! Hadi Kaze anashangaa!

KOCHA Msaidizi wa Yanga, Cedrick Kaze amesema anashangazwa na mashabiki wa soka wanaombeza straika wa timu hiyo, Fiston Mayele baada ya kushindwa kutetema katika mechi mbili mfululizo zilizopita huku akikiri, kwake ndiye mchezaji bora wa msimu.