Gamondi, Skudu wana jambo lao!

Mwanaspoti
Published: Sep 29, 2023 07:03:32 EAT   |  Sports

KAMA wewe ni shabiki wa Yanga na ulikuwa unajiuliza kwanini winga kutoka Sauzi, Mahlatse ‘Skudu’ Makudubela hachezi licha ya kupona kutoka majeraha, basi kuna sapraizi mpya utakayokutana nayo, iwapo mchezaji huyo atapangwa kwenye pambano la marudiano la Ligi ya Mabingwa Afrika wikiendi hii.