Waziri Mkuu aagiza wakaguzi wa Elimu nchini, wakague vitabu hivi, “Lazima tusimamie maadili yetu”

Milard Ayo
Published: Feb 15, 2023 21:07:26 EAT   |  Educational

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza Wakaguzi wa Elimu nchini wapite kwenye shule zote wakakague vitabu vinavyotumika katika shule hizo kama vinaendana na maadili na tamaduni za Kitanzania. Ameyasema hayo leo (Jumatano, Februari 15, 2023) wakati akizungumza na Watumishi wa Mkoa wa Songwe akiwa kwenye majumuisho ya ziara ya kikazi mkoani Songwe ya kukagua miradi ya […]

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza Wakaguzi wa Elimu nchini wapite kwenye shule zote wakakague vitabu vinavyotumika katika shule hizo kama vinaendana na maadili na tamaduni za Kitanzania.

Ameyasema hayo leo (Jumatano, Februari 15, 2023) wakati akizungumza na Watumishi wa Mkoa wa Songwe akiwa kwenye majumuisho ya ziara ya kikazi mkoani Songwe ya kukagua miradi ya maendeleo na mafanikio ambayo Serikali ya awamu ya sita imeyapata katika kipindi cha miaka miwili.