Waziri Makamba: Maneno yanatusaidia yaendelee

Milard Ayo
Published: Jun 01, 2023 17:36:26 EAT   |  News

Ni June 1, 2023 ambapo Waziri wa Nishati, January Makamba amehitimisha Mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Nishati. Miongoni aliyoyazungumza ni kuhusu yale yaliyokuwa yakiendelea mitandaoni. “Haya maneno yanatuongezea hamu na hamasa ya kupata matokeo. Sisi hamasa yetu ni imani ya Mheshimiwa Rais kwetu, hamasa yetu ni matokeo ya kazi yetu kwa uhai wa chama […]

Ni June 1, 2023 ambapo Waziri wa Nishati, January Makamba amehitimisha Mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Nishati.

Miongoni aliyoyazungumza ni kuhusu yale yaliyokuwa yakiendelea mitandaoni.

“Haya maneno yanatuongezea hamu na hamasa ya kupata matokeo. Sisi hamasa yetu ni imani ya Mheshimiwa Rais kwetu, hamasa yetu ni matokeo ya kazi yetu kwa uhai wa chama chetu. Hamasa nyingine ni kuwasaidia Watanzania kwa majukumu tuliyopewa. Lakini hamasa ya mwisho ni maneno haya, mtu akikusema wewe hufai maana yake unajitahidi ili uonekane unafaa. Kwa hiyo haya maneno yanatusaidia. Lakini pia haya maneno yanatusaidia kwa sababu yanawaamsha wanaotupenda na wanaotutakia heri ili watuombee dua na sala.”- Waziri January Makamba

“Maneno haya yanatusaidia kwa sababu yanatufundisha ukomavu, yanatufundisha kuwa na subra, yanatufundisha kuwa na uvumilivu na yanatujenga kuwa viongozi bora zaidi. Sisi tumesema waendelee kwa sababu yanatusaidi. Sisi kisasi chetu ni MATOKEO. Hatutabishana, hatutatupa maneno, hatutajitetea, tutalipa kisasi kwa matokeo” Waziri wa Nishati, January Makamba.