Wapenzi wakamatwa kwa kuiba chupa (45) za mvinyo.!

Milard Ayo
Published: Mar 07, 2023 19:19:28 EAT   |  Travel

Aliyekuwa mlimbwende wa mitindo wa Mexico pamoja na mpenzi wake walihukumiwa kifungo cha miaka minne nchini Uhispania kwa kuiba chupa 45 za mvinyo zenye thamani ya takriban $1.7m (£1.4m). Tukio hilo lilitokea mnamo mwaka 2021 katika hoteli ya kifahari katika jiji la Uhispania la Cáceres, ambapo wanandoa hao walikuwa wakikaa kama wageni. Mahakama iliwataja wanandoa […]

Aliyekuwa mlimbwende wa mitindo wa Mexico pamoja na mpenzi wake walihukumiwa kifungo cha miaka minne nchini Uhispania kwa kuiba chupa 45 za mvinyo zenye thamani ya takriban $1.7m (£1.4m).

Tukio hilo lilitokea mnamo mwaka 2021 katika hoteli ya kifahari katika jiji la Uhispania la Cáceres, ambapo wanandoa hao walikuwa wakikaa kama wageni.

Mahakama iliwataja wanandoa hao kuwa ni Tatania na Estanislao, lakini walitambuliwa na vyombo vya habari vya Uhispania kama Priscila Guevara na Constantín Dumitru.

Kulingana na mahakama, Tatania aliingia katika hoteli ya kifahari ya Atrio mnamo Oktoba 2021 kwa kutumia pasipoti bandia ya Uswizi kisha baadae alijiunga na Estanislao na wote wawili walipata mlo katika mgahawa huo wa Michelin star wakinywa na mvinyo.

Wakati wa  asubuhi na mapema estanislao alirudi ili kuiba mvinyo kwa kutumia ufunguo ulioibwa, wakati ambao Tatania alikuwa mapokezi akizuga.

Miongoni mwa chupa za mvinyo, ambazo waliiba kwenye begi yao, ulikuepo mvinyo wa zabibu ya kifahari ya Karne ya 19 na inaripotiwa kuwa na thamani ya €350,000 (£310,000)

Wizi huo ulizua msako wa polisi wa kimataifa ambao ulikamilika Julai wakati wawili hao walikamatwa walipokuwa wakijaribu kuvuka hadi Croatia.

Wanandoa hao pia wameagizwa kulipa zaidi ya €750,000 kwa uharibifu.

Wakati wa kesi wiki iliyopita, Dumitru alikana mashtaka huku wakili wake, Sylvia Córdoba, akilenga toleo la waendesha mashtaka akisema “Chupa arobaini na tano na taulo nne haziingii kwenye mifuko miwili na zisingeweza kubebwa kirahisi hivyo na mwanamume huyu,”

Guevara alichagua kunyamaza, kulingana na vyombo vya habari vya Uhispania.