Viongozi wa vijiji,kata,Tarafa, na wilaya zaidi ya 150 wapewa Elimu ya utunzaji Mazingira na Vyanzo vya Maji

Milard Ayo
Published: Mar 11, 2023 14:57:31 EAT   |  Educational

Viongozi wa ngazi za vijiji,kata na Wilaya za Korogwe na Handeni zaidi ya mia na hamsini wamepewa Elimu juu ya utunzaji wa Mazingira na usimamizi wa vyanzo vya maji. Akizungumza mara baada ya mafunzo hayo Mratibu wa mradi wa sauti Youth World Vision Shukran Dickson amesema kuwa lengo la kikao hicho ni kuangalia namna bora […]

Viongozi wa ngazi za vijiji,kata na Wilaya za Korogwe na Handeni zaidi ya mia na hamsini wamepewa Elimu juu ya utunzaji wa Mazingira na usimamizi wa vyanzo vya maji.

Akizungumza mara baada ya mafunzo hayo Mratibu wa mradi wa sauti Youth World Vision Shukran Dickson amesema kuwa lengo la kikao hicho ni kuangalia namna bora ya kutatua changamoto ya uharibifu wa Mazingira.

.

“Unajua hapa Korogwe tumekuwa na changamoto kubwa ya uvunaji wa mazao ya misitu hivyo kwasasa tunapitishana ili kufahamu sheria mbalimbali za uvunaji wa mazao ya misitu pamoja na utunzani wa vyanzo vya maji ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi”Alisema Shukran

Aidha shukran alitoa wito kwa viongozi na kuwataka kuzisimamia Sheria zilizo weka na Jumuhuri ya Muungano wa Tanzania za kusimamia Mazingira na kutunza vyanzo vya maji ili hayo mazingira yasiharibike kwani tunapo haribu Mazingira tuna haribu maisha ya kizazi cha sasa na baadaye kwani mazingira ni Uhai.

Hata hivyo amesema kuwa mradi huo wa sauti vijana unao fanyakazi katika Wilaya ya Korogwe na handeni una fadhili na Shirika la Umoja wa AU kwa bajeti ya 1.6 Bilioni kwa miaka mitatu.

.

Kwa upande wake Bob Matunda ambaye ni muhifadhi msaidizi katika msitu wa aman ametoa wito kwa wenye viti wa vijiji kufata taratibu za utunzaji wa mazingira pamoja na vyanzo vya maji kwa kuweka Sheria ndogo ndogo zitakazo wawezesha Wananchi kuto kuvuna misitu wala kuharibu vyanzo vya Maji.

Joyces Malekela Mwandisi wa Maji Ruwasa Wilaya ya Korogwe alisema kuwa kutokana na Uharibifu mkubwa wa Mazingira umepelekea Vyanzo vingi vya Maji kukauka na hivyo kuathiri upatikanaji wa maji kwa wananchi na hivyo ametoa rai kwa Wananchi kutunza Mazingira kwa kupanda miti kwenye vyanzo vya Maji.