Tanesco wamepandishwa Mishahara baada ya miaka 17

Milard Ayo
Published: Jun 01, 2023 17:30:40 EAT   |  News

Ni June 1, 2023 ambapo Waziri wa Nishati, January Makamba amehitimisha Mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Nishati Bungeni Dodoma. “Na wao wanajua wafanyakazi wa TANESCO, kwa mara ya kwanza katika miaka 17 tumewapandishia mishahara majuzi. Miaka 17 hatujapandisha mishahara. Sasa hivi tunapimana kwa matokeo”—Waziri wa Nishati, January Makamba. “Hatutapunguza mtu kazi TANESCO, ila tutawahitaji […]

Ni June 1, 2023 ambapo Waziri wa Nishati, January Makamba amehitimisha Mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Nishati Bungeni Dodoma.

“Na wao wanajua wafanyakazi wa TANESCO, kwa mara ya kwanza katika miaka 17 tumewapandishia mishahara majuzi. Miaka 17 hatujapandisha mishahara. Sasa hivi tunapimana kwa matokeo”—Waziri wa Nishati, January Makamba.

“Hatutapunguza mtu kazi TANESCO, ila tutawahitaji wawe tayari kupokea ujuzi mpya na majukumu mapya yanayoendana na mahitaji ya dunia mpya. Waondoke katika ‘comfort zone’ kwa sababu dunia ya huduma inabadilika. Umeme ni huduma. Kwa hiyo tutawapa mafunzo, tutawawezesha, na tutakuwa nao.” Waziri wa Nishati, January Makamba

Waziri Makamba amesisitiza kwamba yeye anajikita kwenye kuwa karibu na wafanyakazi hao na kuwajengea uwezo badala ya kuwaza kuwafukuza.