Siku ya utabiri wa hali ya hewa duniani.

Milard Ayo
Published: Mar 23, 2023 06:13:18 EAT   |  News

Siku kama ya leo miaka 73 iliyopita, liliasisiwa Shirika la Hali ya Hewa Duniani ‘WMO’. Shirika hilo linafungamana na Umoja wa Mataifa na taasisi zote za hali ya hewa ulimwenguni hushirikiana na shirika hilo. Miongoni mwa malengo ya kuanzishwa shirika hilo ni kutoa msaada wa elimu ya hali ya hewa kwa wataalamu wa anga, mabaharia, wakulima […]

Siku kama ya leo miaka 73 iliyopita, liliasisiwa Shirika la Hali ya Hewa Duniani ‘WMO’. Shirika hilo linafungamana na Umoja wa Mataifa na taasisi zote za hali ya hewa ulimwenguni hushirikiana na shirika hilo.

Miongoni mwa malengo ya kuanzishwa shirika hilo ni kutoa msaada wa elimu ya hali ya hewa kwa wataalamu wa anga, mabaharia, wakulima na shughuli nyingine za kibinadamu.

Ni kwa ajili hiyo ndio maana siku ya leo yaani tarehe 23 Machi ikajulikana kuwa Siku ya Hali ya Hewa Duniani.

Lakini tunapoadhimisha siku hii leo tukumbuke kuwa  iwapo ongezeko la joto duniani litaongeza zaidi marudio na ukubwa wa matukio ya hali mbaya ya hewa.

Ndiyo maana ni lazima tuweke kikomo cha kupanda kwa joto duniani kisizidi nyuzi joto 1.5.” 

Kuweka hai lengo hilo la kusalia na nyuzijoto 1.5 kunahitaji punguzo la asilimia 45 la uzalishaji wa hewa chafuzi duniani ifikapo mwaka 2030 ili kufikia hali ya kutozalisha kabisa hewa ukaa katikati mwa karne hii. Hii ni kumbukumbu tu ya Ujumbe alioutoa katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres mwaka 2022.

Taarifa za hali ya hewa zinalenga katika kusaidia nchi kufikia malengo ya mpango wa Taifa katika kujenga uchumi wa viwanda kwa kusaidia kupunguza athari zitokanazo na majanga yanayosababishwa na hali mbaya ya hewa ili kusaidia kulinda mafanikio ya uwekezaji katika miundo mbinu ya uchukuzi.

Siku zote majanga ya asili hayawezi kuepukika, lakini taarifa kutoka kwa kila mmoja wetu zikiwafikia walengwa kabla ya janga husika kutokea basi zitasaidia kujipanga ili kukabiliana na madhara yanayoweza kujitokeza.