Siku ya Maji Duniani Wateraid watoa kauli hii “Mpango wa miaka 5, tunamaliza kero ya maji”

Milard Ayo
Published: Mar 22, 2023 10:53:13 EAT   |  News

Katika kuadhimisha siku ya Maji Duniani, Shirika la WaterAid Tanzania linatarajia kuzindua mkakati wenye matarajio ya miaka mitano (2023-2028) kwa lengo la kumaliza tatizo la maji na usafi wa mazingira. Akizungumza leo, Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la WaterAid, Anna Mzinga amesema..”Kwa wasichana, upatikanaji wa vifaa vya WASH ni jambo muhimu linaloathiri mahudhurio ya shule, hasa […]

Katika kuadhimisha siku ya Maji Duniani, Shirika la WaterAid Tanzania linatarajia kuzindua mkakati wenye matarajio ya miaka mitano (2023-2028) kwa lengo la kumaliza tatizo la maji na usafi wa mazingira.

Akizungumza leo, Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la WaterAid, Anna Mzinga amesema..”Kwa wasichana, upatikanaji wa vifaa vya WASH ni jambo muhimu linaloathiri mahudhurio ya shule, hasa wakati wa hedhi na ni moja ya sababu kuu za wasichana kuacha shule.

Asilimia 34 ya wasichana waliripoti kukosa shule wakati wa hedhi kutokana na ukosefu wa vyumba vya kubadilishia nguo na asilimia 26 walilaumu ukosefu wa choo safi na kinachofaa.

“WaterAid, tutaendelea kushirikiana na washirika ili kuunga mkono na kushawishi sera na bajeti na kuchangia katika kuboresha upatikanaji wa huduma salama, nafuu, zinazozingatia jinsia, Jumuishi kijamii na endelevu, huduma za maji taka na Usafi kwa kila mtu, kila mahali,”amesema.

“Tunajua kwamba upatikanaji unaotegemewa wa maji na usafi wa mazingira unaosimamiwa kwa usalama, pamoja na desturi na rasilimali za usafi wa kiafya, huwawezesha watoto, familia na jamii kuwa msingi wa kudumu wa kuboresha afya, uchumi imara na fursa kubwa zaidi,”. Anna Mzinga

“Tunatamani kuwa mahali ambapo hakuna jamii inayorudishwa nyuma na magonjwa yasiyo kwisha yanaosababishwa na miondombinu mibovu ya maji taka, afya na usafi wa mazingira,”. Anna Mzinga

Katika hatua nyingine Mzinga amesema, msichana anaweza kutengwa na maisha bora kwa sababu shule yake haina vyoo vinavyofanya kazi vilivyo na milango ya kufunga au chumba cha usafi wa hedhi.