Serikali ya Wanafunzi chuo Kikuu Huria wampongeza hili Rais Samia

Bunge la Serikali ya Wanafunzi wa chuo Kikuu Huria Tanzania limepongeza Juhudi na jitihada zilizofanywa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan katika utumishi wake kwa miaka miwili ya Uongozi wake. Tamko hilo limetolewa leo Mkoani Manyara katikaKikao Cha 42 Cha Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUTSO). […]
Bunge la Serikali ya Wanafunzi wa chuo Kikuu Huria Tanzania limepongeza Juhudi na jitihada zilizofanywa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan katika utumishi wake kwa miaka miwili ya Uongozi wake.
Tamko hilo limetolewa leo Mkoani Manyara katikaKikao Cha 42 Cha Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUTSO).
Spika wa bunge Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu Huria na Rais Bwana Felix Lugeiyamu amesema Rais Samia ameboresha Mambo mbalimbali nchini ikiwemo demokrasia ya Vyama vya Siasa,Uhuru wa habari pamoja na kuongeza idadi ya vyema za mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, huku akisema wapo tayari kutumwa wakati wowote na kubeba maono na Malengo ya Rais
Nae Aziza Mussa kutoka Zanzibar ametumia nafasi hiyo kukuomba Rais Samia kuwajengea chuo kikubwa cha Open University Zanzibar kwa kuwa kilichopo sasa ni matawi pekee.
“Tunaona vyuo vingi vikuu Zanzibar vipo vikubwa vizuri lakini Open University kwa bahati mbaya hakipo Zanzibar lipo tawi pekee”