RPC geita anena ‘Vijana hawaendi Makanisani, Misikitini na kwenye mizimu’

Milard Ayo
Published: May 31, 2023 12:31:25 EAT   |  General

Imeelezwa kuwa Mmomonyoko wa Maadili kwa Vijana umekuwa ukisababishwa na Baadhi ya Vijana ambao wamekuwa wakiukwaji wa Maadili ambapo changamoto hiyo imekuwa ikichangiwa na Baadhi ya Wazazi kutohimiza watoto wao kuwa na hofu ya Mungu ikiwemo kutokwenda katika Nyumba za Ibada pamoja na kukiuka Mila na Desturi za Kiafrika. Akizungumza katika kongamano la Vijana lililoandaliwa […]

Imeelezwa kuwa Mmomonyoko wa Maadili kwa Vijana umekuwa ukisababishwa na Baadhi ya Vijana ambao wamekuwa wakiukwaji wa Maadili ambapo changamoto hiyo imekuwa ikichangiwa na Baadhi ya Wazazi kutohimiza watoto wao kuwa na hofu ya Mungu ikiwemo kutokwenda katika Nyumba za Ibada pamoja na kukiuka Mila na Desturi za Kiafrika.

Akizungumza katika kongamano la Vijana lililoandaliwa na Mkuu wa wilaya ya Mbogwe ,Bi.Sakina Mohamed kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika wilaya hiyo liliofanyika katika Viwanja vya Masumbwe wilayani humo Kamanda wa Jeshi la Polosi Mkoa wa Geita , Kamishina Msaidizi Safia Jongo amesema Mmomonyoko wa Maadili kwa Vijana umekuwa ukichangiwa na Wazazi pamoja na Teknolojia .

“Vijana wengi hawaendi Makanisani hawaendi Misikitini wala hawaendi kwenye Mizimu kweli si kweli ee wasukuma huwa mnamizimu kutokana na watoto kukosa Maadili tumepata kizazi ambacho kina matendo na Matukio ya ukatili yaliyopitiliza Matokeo ya wazazi kukosa Mda kuwapa watoto elimu imechangia watoto wengi kuwa waharifu ,” RPC, Jongo.

Akifunga kongamano la Vijana wilayani humo Mkuu wa Mkoa wa Geita ,Martine Shigella amewahasa vijana kufany kazi kwa Bidii juu ya fursa zinzopatikana katika wilaya hiyo huku akitoa Maagizo kwa Halmashauri kuhakikisha inasajili vikundi na kuwapa Mikopo kw ajili ya kujikwamua huku akitoa kiasi cha shilingi Milioni 5 kwa kikundi cha Vijana wilayani humo.

Naye Mkuu wa wilaya ya Mbogwe Bi, Sakina Mohamed amempongeza Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha katika wilaya hiyo kwa ajili wananbogwe pamoja na vijana ambao wamekuwa wakishirikiana nao katika kuleta fursa kwa vijana wilayani humo.

Bi.Sakina George Balele ameendelea kumpongeza Mkuu wa wilaya ya Chato Ndg.Deusdediti Katwale kwa kuhudhulia kongamano hilo ambalo alitoa fedha kwa ajili ya kusaidia kikundi cha vijana ambacho kimekuwa kikihitaji kujikwamua kiuchumi.

Mobahe amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Geita katika kuendelea kushirikiana na Serikali kuiomba Halmashauri ya wilaya hiyo kutenga maeneo kwa ajili ya kilimo ,Ufugaji pamoja na Mikopo ya fedha ili kusaidia vikundi ambavyo vimesajiliwa na Halmashauri ili kuwakwamua kiuchumi.