Rapa Snoop Dogg azindua lebo yake mpya ya kahawa “INDOxyz”

Milard Ayo
Published: Mar 17, 2023 10:51:21 EAT   |  Business

Rapa na mjasiriamali Snoop Dogg ameamua kupanua  himaya yake ya biashara tena, wakati huu akijikita katika safu ya bidhaa bora za kahawa na maharagwe yanayopatikana nchini Indonesia. Ameshirikiana na mjasiriamali wa kahawa wa Kiindonesia Michael Riady kuzindua INDOxyz.    “biashara hii ni ya kiwango cha juu kwani ni kahawa  iliyoundwa kwa ajili ya kizazi kijacho […]

Rapa na mjasiriamali Snoop Dogg ameamua kupanua  himaya yake ya biashara tena, wakati huu akijikita katika safu ya bidhaa bora za kahawa na maharagwe yanayopatikana nchini Indonesia.

Ameshirikiana na mjasiriamali wa kahawa wa Kiindonesia Michael Riady kuzindua INDOxyz.   

“biashara hii ni ya kiwango cha juu kwani ni kahawa  iliyoundwa kwa ajili ya kizazi kijacho cha wajasiriamali na wavumbuzi,” kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari iliyotumwa kwa CNN.

Snoop Dogg, ambaye jina lake halisi ni Calvin Broadus, alisema

“Uhusiano wangu na kahawa unarudi nyuma kabisa, maranyingi upo katika studio ukifanya hit baada ya kuchoka basi kahawa ilitoa motisha ambayo ilitufanya tuendelee baada ya kuitumia”

“Leo tunaadhimisha uzinduzi wa kampuni mpya niliyounda pamoja na mshirika wangu Michael, ambaye alinitambulisha kwenye soko la kahawa ya Kiindonesia yenye ladha nzuri zaidi,” alisema.

Snoop aliongeza: “Indo itabadilisha tasnia, ninaweza kukuahidi hilo,” akimaanisha chapa /label yake ya kahawa, ambayo pia ni kifupi cha kawaida cha Indonesia Nchi ambayo ni mzalishaji mkuu wa kahawa duniani.

pamoja na kutoa zaidi ya albamu kumi na mbili za studio na kupokea tuzo kadhaa za Grammy kama rapa, Snoop Dogg amekuwa akipanua himaya yake ya biashara.

Mnamo 2020, alizindua lebo yake ya mvinyo.