Rais wa BMMT atangaza Uteuzi, Gwajima, mzee wa upako watajwa

Milard Ayo
Published: Feb 20, 2023 19:23:50 EAT   |  Business

Rais wa Baraza la Manabii na Mitume Tanzania (BMMT) Dr.Joachim Peter ametangaza Uteuzi Mpya wa Viongozi watakaoendesha Shughuli zote za Utendaji Ndani ya Baraza hilo. Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam amesema kuwa amemteua Prophert Godson kuwa mwenyekiti wa idara ya fedha na mipango Taifa huku engineer Methew Mwalukira kuwa Naibu wake […]

Rais wa Baraza la Manabii na Mitume Tanzania (BMMT) Dr.Joachim Peter ametangaza Uteuzi Mpya wa Viongozi watakaoendesha Shughuli zote za Utendaji Ndani ya Baraza hilo.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam amesema kuwa amemteua Prophert Godson kuwa mwenyekiti wa idara ya fedha na mipango Taifa huku engineer Methew Mwalukira kuwa Naibu wake katika idara hiyo.

Dr.Joachim Peter, amemteu Christina Felix Sengoma kuwa Mwenyekiti wa idara ya uinjilisti Taifa huku Makamu wake ni Prophet Justine Muingereza.

Dr.Joachim Peter amemteua Mtumishi wa wangu Aposto Suleisoni Elikana kuwa Mwenyekiti wa idara ya Ulinzi na Usalama huku Makamu wake ni Aposto peter Lukuta
Mtume na Mwalimu Emmanuel Charles ameteuliwa kuwa mtu wa maadili na nidhani huku akisaidiana na nabii Honest Malya.

Rais wa Baraza la Manabii na Mitume Tanzania (BMMT) Dr.Joachim Peter ameendelea kufanya mabadiliko ya wasaidizi wa kanda mbalimbali katavi,Kilimanjaro, Iringa, Dar es salaam

Aidha Rais wa Baraza la Manabii na Mitume Tanzania (BMMT) Dr.Joachim Peter amesema kuwa Baraza la mitumie na manabii Tanzania linawalezi ambao ni Dr Bishop Gwajima, Mzee wa Upako Mchungaji Lusekela, mtumishi wa mungu Dastuni haule Maboya n.k.

“tumekuwa na umuhimu sana Taifa letu kutambua hizi huduma 5 hasa huduma kubwa ambazo zimebeba msingi wa kanisa huduma ya mitume na manabii, misingi ya huduma hii nikuinu watu wenye huduma change au zinazoanza”