Rais Samia awataka TADB kuwezesha Program za Vijana

Milard Ayo
Published: Mar 21, 2023 06:09:40 EAT   |  Business

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameipongeza Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa kazi nzuri inayoifanya na kuiasa kuendelea kuwezesha programu ya vijana ya kilimo biashara ‘Building a Better Tomorrow’ BBT kwa kupatia washiriki wake zana na vitendea kazi vya kilimo kwa muda wa miaka mitatu mfululizo […]

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameipongeza Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa kazi nzuri inayoifanya na kuiasa kuendelea kuwezesha programu ya vijana ya kilimo biashara ‘Building a Better Tomorrow’ BBT kwa kupatia washiriki wake zana na vitendea kazi vya kilimo kwa muda wa miaka mitatu mfululizo wa programu hiyo.

Rais Samia alitoa pongezi hizo wakati akikagua zana na vitendea kazi vya kilimo vilivyotolewa na TADB Chinangali, Wilaya ya Chamwino kwa ajili ya uzinduzi wa mashamba makubwa ya pamoja (block farming) iliyo chini ya programu hiyo.

TADB imetoa zaidi ya shilingi milioni mia tano kununua zana na vitendea kazi vya kilimo kwa ajili ya vijana 812 waliojiunga na programu hiyo kwa awamu hii ya kwanza.