Rais Mwinyi akutana na Balozi wa Ufilipino nchini Tanzania

Milard Ayo
Published: Mar 02, 2023 17:40:33 EAT   |  Travel

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar ina mengi ya kujifunza uzoefu na weledi kutoka nchi ya Ufilipino hasa kwenye sekta za mafuta na gasi ,afya, utalii na uvuvi . Pia Dk.Mwinyi amemuomba Balozi wa Ufilipino kuitangaza Zanzibar katika fursa mbalimbali ambazo zinapatikana visiwa humo. Dk.Mwinyi aliyasema […]

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar ina mengi ya kujifunza uzoefu na weledi kutoka nchi ya Ufilipino hasa kwenye sekta za mafuta na gasi ,afya, utalii na uvuvi .

Pia Dk.Mwinyi amemuomba Balozi wa Ufilipino kuitangaza Zanzibar katika fursa mbalimbali ambazo zinapatikana visiwa humo.

Dk.Mwinyi aliyasema hayo leo tarehe 02 Machi, 2023 Ikulu   Zanzibar  alipokutana  na Balozi wa Ufilipino Tanzania  ,Marie Charlotte  G.Tang aliyefika kujitambulisha.

Naye, Balozi Marie Charlotte G.Tang amesema  ataongeza  uhusiano kati ya Ufilipino na Tanzania pia amekubali kuitangaza na kuwashawishi wawekezaji kutoka nchini mwake kuja Zanzibar kuangalia fursa za Uwekezaji zinazopatikana kutokana na kufanana mazingira kati ya  Ufilipino na Zanzibar.

.
.
.
.
.