Rafiki wa MC aliyejirusha ghorofani atoweka, aacha ujumbe mzito (+video)

Milard Ayo
Published: May 31, 2023 17:17:45 EAT   |  General

Ni siku 7 zimepita tangu Joel Misesemo (MC Joel) ajirushe kutoka ghorofa 7 Makumbusho DSM. Leo AyoTV imepata taarifa juu ya Rafiki wa karibu wa MC JOEL, aitwaye Tyson Nduguru nae ametoweka anatafutwa na Familia yake. Maswali yaliyozua mjadala ni Inakuwaje rafiki yake ajirushe ghorofani May 23,2023, nae apotee May 26, 2023 akiwa ameaga anaenda […]

Ni siku 7 zimepita tangu Joel Misesemo (MC Joel) ajirushe kutoka ghorofa 7 Makumbusho DSM.

Leo AyoTV imepata taarifa juu ya Rafiki wa karibu wa MC JOEL, aitwaye Tyson Nduguru nae ametoweka anatafutwa na Familia yake.

Maswali yaliyozua mjadala ni Inakuwaje rafiki yake ajirushe ghorofani May 23,2023, nae apotee May 26, 2023 akiwa ameaga anaenda msibani kwa rafiki yake?

Pia jumbe mbili nzito za mwisho zenye mafumbo katika ukurasa wake facebook zinaongeza maswali pia.

AyoTV imefanya mahojiano Mkewe ambaye anahangaika kumtafura Mumewe Kwenye Wodi za Wagonjwa, movhwari na hata vituo vya Polisi.