Nyota wa RnB R.kelly huenda akaachiwa huru akiwa na miaka 100!

Milard Ayo
Published: Feb 23, 2023 04:45:37 EAT   |  Entertainment

Nyota wa muziki wa RnB aliyegeuka kuwa mhalifu maarufu kama R.Kelly imesemekana kuwa hatoweza kuachiliwa hadi 2066, yaani mwaka mmoja kabla ya kutimiza miaka 100, ikiwa jaji wa shirikisho atakubali mapendekezo ya waendesha mashtaka katika kesi yake ya hukumu Ya alhamis katika mji wa Chicago. Kelly, 56, atahukumiwa kwa makosa yake kutoka mwaka jana huko […]

Nyota wa muziki wa RnB aliyegeuka kuwa mhalifu maarufu kama R.Kelly imesemekana kuwa hatoweza kuachiliwa hadi 2066, yaani mwaka mmoja kabla ya kutimiza miaka 100, ikiwa jaji wa shirikisho atakubali mapendekezo ya waendesha mashtaka katika kesi yake ya hukumu Ya alhamis katika mji wa Chicago.

Kelly, 56, atahukumiwa kwa makosa yake kutoka mwaka jana huko Chicago ya ponografia ya watoto na ushawishi wa kingono na tayari anatumikia miaka 30 kwa hatia zake za ulaghai na biashara ya ngono 2021 huko New York.

Katika memo ya hukumu wiki iliyopita, walipendekeza Kelly kutumikia miaka 25 zaidi Waendesha mashtaka walimtaja Kelly kama “mnyanyasaji wa kingono” ambaye alitumia umaarufu na utajiri wake kuwashawishi mashabiki wakubwa kuwanyanyasa kingono na kisha kuwatupilia mbali. Wanasema hajaonyesha kujuta.

Majaji huko Chicago walimtia hatiani Kelly kwa makosa matatu kila moja ya kutengeneza ponografia ya watoto na kuwashawishi watoto kufanya ngono huku ikisemekana kuwa Kelly alifutiwa mashtaka kwa madai kuwa alifanikiwa kuiba kesi yake ya mwaka 2008 kuhusu ponografia ya watoto.
Iwapo mwimbaji ataagizwa kutumikia kifungo kimoja baada ya kingine, hilo lingefuta nafasi yoyote ya Kelly kutoka gerezani akiwa hai.