Ndani ya siku moja zaidi ya Bilioni 2 Zachangwa, Musukuma atangaza kuanzishwa kwa Benki ya madini

Milard Ayo
Published: May 30, 2023 15:15:24 EAT   |  Sports

Wachimbaji madini Tanzania wameazimia kuanzisha benki yao itakayowawezesha kuwapa mtaji wa kuchimba madini yao ambapo leo wameweza kuchangishisha zaidi ya billion mbili za kitanzania baada ya wachimbaji hao 102 kukutana kwenye jiji la Arusha. Rais wa shirikisho la vyama vya wachimbaji madini Tanzania (Femata) John Bina ameyasema hayo jijini Arusha leo jumanne Mei 30 kwenye […]

Wachimbaji madini Tanzania wameazimia kuanzisha benki yao itakayowawezesha kuwapa mtaji wa kuchimba madini yao ambapo leo wameweza kuchangishisha zaidi ya billion mbili za kitanzania baada ya wachimbaji hao 102 kukutana kwenye jiji la Arusha.

Rais wa shirikisho la vyama vya wachimbaji madini Tanzania (Femata) John Bina ameyasema hayo jijini Arusha leo jumanne Mei 30 kwenye kikao cha wachimbaji madini cha kujadili uanzishwaji wa benki hiyo.

Rais Bina amesema uanzishwaji wa benki hiyo utajibu changamoto mbalimbali za wachimbaji na wadau wote wanaonufaika na mnyororo wa thamani ya madini.

Mkurugenzi mtendaji wa shirika la madini la Taifa (Stamico) Dk Venance Mwasse amesema uanzishwaji wa benki hiyo ni maendeleo makubwa na umuhimu hasa kwa wachimbaji wadogo nchini kwani hawana mitaji.

Dk Mwasse amesema wazo la uanzishaji wa benki ni zuri kwani hata mataifa mengine ya nje yataiga kwenu kwani mmetegua mtego mkubwa wa kuwa na benki yenu.

Mbunge wa Geita vijijini, Joseph Musukuma ambaye amewawakilisha wabunge wanaotoka kwenye maeneo yenye migodi amesema uanzishwaji wa benki hiyo ni wazo zuri litakuwa kimbilio kwa wachimbaji nakusema wanatarajia kupeleka wazo hilo kwa Rais wa Tanzania kwa ajili yakuanza kwa harambee.

Mchimbaji maarufu wa madini ya Tanzanite, Bilionea Saniniu Laizer amesema uwepo wa benki hiyo itakuwa fursa kubwa kwa wachimbaji.