NATO inajadili ‘dhamana ya usalama’ kwa Ukraine

Milard Ayo
Published: Jun 01, 2023 08:33:24 EAT   |  General

Uvamizi wa Urusi nchini Ukraine mwezi Februari mwaka jana umeupa nguvu muungano wa kijeshi wa nchi za Magharibi ulioanzishwa takriban miaka 75 iliyopita kukabiliana na Umoja wa Kisovieti lakini kwa zaidi ya wiki tano tu kabla ya mkutano wa kilele wa viongozi wa NATO katika mji mkuu wa Lithuania Vilnius kuna migawanyiko katika masuala muhimu. […]

Uvamizi wa Urusi nchini Ukraine mwezi Februari mwaka jana umeupa nguvu muungano wa kijeshi wa nchi za Magharibi ulioanzishwa takriban miaka 75 iliyopita kukabiliana na Umoja wa Kisovieti lakini kwa zaidi ya wiki tano tu kabla ya mkutano wa kilele wa viongozi wa NATO katika mji mkuu wa Lithuania Vilnius kuna migawanyiko katika masuala muhimu.

Kuu miongoni mwao ni msukumo wa Kyiv kujiunga na NATO, shirika ambalo linahitaji maridhiano kufanya maamuzi.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, akiungwa mkono na nchi za NATO mashariki mwa Ulaya, anatoa wito wa “ujumbe wa wazi” katika mkutano wa kilele wa Julai kwamba Kyiv itajiunga mara tu vita na Urusi vitakapomalizika.

Lakini wanadiplomasia kutoka nchi za NATO wanasema mamlaka yake kuu ya kijeshi, Marekani, inasita kwenda mbali zaidi ya kiapo cha 2008 kwamba Ukraine siku moja itakuwa mwanachama.

Kujiunga na NATO kungemaanisha Ukraine itafunikwa na kifungu cha 5 cha ulinzi wa pamoja cha muungano huo ambacho kinawalazimu washirika wote kusaidia kuilinda ikiwa itashambuliwa.

Hii leo rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky aliwasili Moldova kwenye  mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Kisiasa ya Ulaya kwa lengo la kujadili matumaini ya Kyiv ya kujiunga na Umoja wa Ulaya na muungano wa kijeshi wa NATO.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema amesafiri kwenda Moldova kuhudhuria mkutano wa kilele wa Alhamisi wa Jumuiya ya Kisiasa ya Ulaya, ambao unatazamiwa kuhudhuriwa na makumi ya viongozi, na kwamba atakuwa na mikutano mingi ya nchi mbili.

Zelensky alisema anafanya kazi ya kujenga uungwaji mkono kwa muungano wa mamlaka ya kusambaza ndege za kivita ili kuisaidia Ukraine kuviondoa vikosi vya Urusi, na kwamba atajadili pia mpango wake wa amani pamoja na matarajio ya Kyiv kujiunga na NATO na Umoja wa Ulaya.