Mwili waopolewa mto Msimbazi DSM, Jeshi la Zimamoto (VideO+)

Milard Ayo
Published: Mar 22, 2023 15:56:26 EAT   |  Sports

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Ilala Dar es Salaam limeopoa mwili wa mwanaume mmoja katika mto msimbazi maeneo ya Jangwani akiwa amefariki baada ya kusombwa na maji siku ya jumapili akijaribu kuvuka mto maeneo ya karakata saa kumi na moja jioni na maji kumshindwa na kupoteza maisha. Akiongea na Ayo tv Kaimu Mkuu […]

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Ilala Dar es Salaam limeopoa mwili wa mwanaume mmoja katika mto msimbazi maeneo ya Jangwani akiwa amefariki baada ya kusombwa na maji siku ya jumapili akijaribu kuvuka mto maeneo ya karakata saa kumi na moja jioni na maji kumshindwa na kupoteza maisha.

Akiongea na Ayo tv Kaimu Mkuu wa Uokozi majini Dar es salaam Omary Katonga amesema mtu huyo imebainika kua alikuwa Mfanyabishara katika Soko la Karume na siku hiyo alikuwa akitoka katika biashara zake na ndugu zake wameshamtambua na Umri wake ni miaka 41.

Ikumbukwe tarehe 19 mwezi huu siku ya jumapili mkoa wa Dar es salaam ulipata mvua kubwa maeneo mbalimbali ambayo yalileta athari huku mamlaka ya hali ya hewa nchini TMA ikitoa tahadhali ya kuwepo kwa mvua kubwa na wananchi kuchukua tahadhari zote za kujikinga.