Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Wilaya ya Moro anena haya

Milard Ayo
Published: Sep 06, 2023 09:05:04 EAT   |  Jobs and Career

Mwenyekiti chama cha walimu Wilaya ya Morogoro Vijijini Mkoa Morogoro Mwalimu Mbaruku Chipeta amewataka walimu wilayani humo kufanya kazi kwa bidii ili kupandisha kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi Mwalimu Chipeta ameyasema hayo wakati akizungumza na walimu wa ajira mpya 107 wa mwaka 2023 katika semina maalum iliyolenga kuwajengea uwezo na kuwapa hamasa ya ufundishaji ili […]

Mwenyekiti chama cha walimu Wilaya ya Morogoro Vijijini Mkoa Morogoro Mwalimu Mbaruku Chipeta amewataka walimu wilayani humo kufanya kazi kwa bidii ili kupandisha kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi

Mwalimu Chipeta ameyasema hayo wakati akizungumza na walimu wa ajira mpya 107 wa mwaka 2023 katika semina maalum iliyolenga kuwajengea uwezo na kuwapa hamasa ya ufundishaji ili kuinua kiwango cha ufaulu

Amesema mwaka 2023 serikali imeajiri jumla ya walimu wapya 107 wa shule za msingi na sekondari hivyo lazima watambue dhamira ya serikali ni kuhakikisha watoto wanapata haki yao ya kielimu

Aidha amewataka kuacha kujiingiza katika vitendo vya kihalifu ambavyo vinaweza kuwaharibia ajira zao ikiwemo uvujishaji mitihani,mapenzi na wanafunzi pamoja utoro kazini badala yake wawe wamoja katika kushirikiana kwenye kazi

Kuhusu suala la malipo ya fedha za kujikimu Mwenyekiti amesema tayari chama cha walimu (CWT) kimeishafanya jitihada za karibu na mwajiri wao ili kuhakikisha stahiki za walimu zinalipwa kwa wakati

Naye Katibu wa CWT Wilaya ya Morogoro vijijini Mwalimu Jane Shoo amesisitiza suala la uwajibika kwani hakuna haki bila wajibu hivyo wakati wakishughulikiwa kutafuta ufumbuzi wa Changamoto zao lazima watambue wanawajibu wakufanya kazi kwa bidii.

Nao baadhi ya walimu ambao wamehudhuria semina hiyo wamekishukuru chama cha walimu Wilaya ya Morogoro vijijini kwa kuwapa mwanga katika kazi yao huku wakiahidi kujiunga na chama hicho pamoja na kufanya kazi kwa bidii.

.
.
.
.
.