Muda wa kusitisha mapigano nchini Sudan warefushwa kwa siku 5

Milard Ayo
Published: May 30, 2023 11:26:17 EAT   |  News

Saudi Arabia na Marekani ambazo ni wapatanishi katika mzozo wa Sudan kati ya jeshi na kikosi cha msaada wa dharura RSF zimekaribisha makubaliano hayo mapya ya kuongeza muda wa usitishaji mapigano wakati Wasudan milioni 25 kati ya 45 wanahitaji misaada ya kibinadamu ili kuendelea kuishi. Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imeendelea kueleza kwamba, […]

Saudi Arabia na Marekani ambazo ni wapatanishi katika mzozo wa Sudan kati ya jeshi na kikosi cha msaada wa dharura RSF zimekaribisha makubaliano hayo mapya ya kuongeza muda wa usitishaji mapigano wakati Wasudan milioni 25 kati ya 45 wanahitaji misaada ya kibinadamu ili kuendelea kuishi.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imeendelea kueleza kwamba, kurefushwa kwa muda huo kutatoa fursa ya usafirishaji wa misaada ya kibinadamu, kuregeshwa kwa huduma muhimu na nafasi ya kufanyika mazungumzo juu ya suluhisho la muda mrefu kuhusu mzozo huo.

Vita vilivyoanzishwa tarehe 15 Aprili kati ya jeshi la Jenerali Abdel Fattah al-Burhane na wanamgambo wa Rapid Support Forces (FSR) kiosi kinachoongozwa na Jenerali Mohamed Hamdane Daglo vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 1,800 na karibu watu milioni moja na nusu kuyahama makazi yao na wengie kukimilia nje ya nchi.

Milio ya risasi bado ilisikika mjini Khartoum Jumatatu jioni, wakaazi walisema, huku RSF ikilishutumu jeshi kwa kufanya mashambulizi mabaya ya anga wakati wa mchana.

Licha ya makubaliano hayo ya kusitisha mapigano kutozingatiwa kikamilifu, takriban Wasudan milioni mbili wamepokea misaada ya kibinadamu  katika siku za hivi karibuni.